This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, 20 February 2015

Huyu ndiye mkuu mpya wa wilaya ya Iramba mh. LUCY MAYEMBA aliyeteuliwa na J.K. Sema neno lolote kwa uteuzi huu


Huyu ndiye mkuu mpya wa wilaya ya Iramba mh. LUCY MAYEMBA aliyeteuliwa na J.K.
Sema neno lolote kwa uteuzi huu

Wanasayansi wamegundua kwamba wanaume walio wakarimu na wanaowasikiza wake zao kidole chao cha nne ni kirefu ikilinganishwa na kidole chao cha pili


Wanasayansi wamegundua kwamba wanaume walio wakarimu na wanaowasikiza wake zao kidole chao cha nne ni kirefu ikilinganishwa na kidole chao cha pili.

Je, unakubaliana na utafiti huu uliofanywa na wanasayansi katika chuo kikuu cha McGill University nchini Canada.

Thursday, 19 February 2015

FUNDI SAA APOKEA KICHAPO BAADA YA KUDAIWA KUMLAWITI MTOTO HUKO ARUSHA

Njemba mmoja ambaye ni fundi saa maeneo ya Stendi Kuu jijini Arusha leo amepokea kipigo cha mbwa mwizi baada ya kudaiwa kumlawiti mwanafunzi wa kiume wa darasa la tatu wa shule moja jijini humo.

Mapigano ya Magaidi na Polisi Mapango ya Amboni Tanga Hii ndio..........


Mapigano ya Magaidi na Polisi Mapango ya Amboni Tanga Hii ndio Full Story

NI kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video wakizungumzia uhalifu....


Cha ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya  Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.

MASHUHUDA WA MAPIGANO 
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili hivi.

“Mke wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi. Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia tena.”

WAZIKIMBIA NYUMBA 
Mwanahawa Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.”

SIKU MBILI HAKUNA KULALA 
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.

“Mimi na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.

INAVYODAIWA 
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu nchi jirani ya Kenya.

Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.

“Lengo lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.

“Yule jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.

WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.

“Kutuambia wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?” alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.

Kusema ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally, mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.

KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.




Watu hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.

KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
“Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,  askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.    

Thursday, 12 February 2015

UN yailaumu Tanzania kwa yanayotokea DRC

Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo.
Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.
Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania
Lakini wachunguzi wa Umoja wa mataifa walipoiuliza serikali ya Tanzania kujibu madai haya ilikanusha kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi yake na wapiganaji wa FDLR.
Umoja wamataifa umesema pia kuwa una ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Ripoti hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yao ya kusalimisha silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.
UN inasema kuwa FDLR wamewatuma wazee waliodhoofika kiafya pekee kujisalimisha na kukabidhi silaha chache sana ambazo zina hitilafu.
Kundi la FDLR, liliundwa mwaka wa 2000 na wahutu waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.Kundi hilo linapinga utawala wa kitutsi na ushawishi wake katika eneo la maziwa makuu.
Rwanda imekuwa ikitazama kundi hilo kama tisho kubwa kwa utawala uliopo na kwa kauli moja na Umoja wa mataifa imekuwa ikishinikiza kupokonywa silaha kwa wapiganaji wake.
Ripoti hiyo pia imetoa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na wanajeshi wa Burundi katika Kivu ya Kusini .
Wataalamu hao wa Umoja wa mataifa wamependekeza serikali za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zifanyie uchunguzi madai hayo ambayo wanasisitiza yalifanywa namajeshiya Burundi pamoja na kikundi cha vijana wapiganaji wajulikanao kama Imbonerakure.

zanzibar SAUTI ZA BUSARA......

Alikiba akiwa tayari kwa ajili ya SAUTI ZA BUSARA Zanzibar..... Makamuzi yanaendelea...

Serikali yaiagiza TANESCO kushusha bei ya umeme

Serikali yaiagiza TANESCO kushusha bei ya umeme

Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene amelitaka shirika la umeme nchini (TANESCO) kupunguza bei ya umeme kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Soma Zaid hapa
Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene amelitaka shirika la umeme nchini (TANESCO) kupunguza bei ya umeme kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam leo mara baada ya kukutana na wafanyabiashara wa mafuta nchini Mh. Simbachawene pia ameishauri mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa
nchi kavu na majini SUMATRA kuona uwezekano wa kupunguza bei za nauli ili wananchi waone faida ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Amesema kwa kuwa bei hizo zinapopanda wananchi wamekuwa wakiilalamikia serikali, ni bora pia wakaishukuru serikali kwa kuonja manufaa ya kushuka kwa bei ya nishati hiyo.
Aidha katika hatua nyingine Waziri huyo wa nishati na madini ameitaka mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji nchini EWURA kuhakikisha inashirikiana na jeshi la polisi
kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ambao kwa sasa umeonekana kufanyika na Ewura pekee bila ya kulishirikisha jesbi la polisi

Saturday, 7 February 2015

JE WEST HAM ATAKUFA KWELI KWA KIKOSI HIKI????? TOA MAONI YAKO


HARRY KANE WA SPURS AENDELEA KUWA TISHIO KWA TIMU KUBWA UINGEREZA........ Aipiga Arsenal...

Kane raiya wa England anaendelea kua tishio na kung'aa baada ya kuilaza arsenal kwa mabao mawili,,,,

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA INDIA KWENYE SHOW YA DIAMOND

Hii ni moja ya picha ya msanii wa kizazi Kipya Naseeb Abdul marufu kama Diamond alipokua akifanya shoo India jana usiku.. shoo ilikua poa sanaa

Rose Ndauka: Sitazaa Tena Nje ya Ndoa

DIVA wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa alikosea kuzaa nje ya ndoa, na sasa hana mpango huo tena.
Rose alisema suala la ujauzito wakati mwingine linaweza kumjia mtu bila kupenda lakini kwa sasa atajitahidi kuona anazaa akiwa ndani ya ndoa.
“Lolote linaweza kutokea lakini kiukweli kwa sasa nitakuwa makini kidogo na ninamuomba Mungu anisaidie mtoto wa pili nimzalie ndani ya ndoa,” alisema Rose ambaye alizaa na Mbongo Fleva, Malick Bandawe kisha kumwagana.
Mwigizaji huyo kwa sasa ameandaa jarida lake ambalo litakuwa linatoka mtaani kila Jumatatu.
GPL

Aunt: Mimba Yangu Siyo ya Waziri!

Muigizaji  wa filamu Aunt Ezekiel Grayson amevunja ukimya na kupinga vikali tetesi za ujauzito wake kuhusishwa na mmoja wa mawaziri wa sasa wa maliasili na utalii  akibainisha kuwa jambo hilo linautesa moyo wake.
Akizungumza na GPL, Aunt alifunguka kwamba, mbali na kumzushia juu ya ujauzito huo, kuwa mara ya kwanza watu asiowajua walieneza uvumi kuwa alikwenda nchini Marekani na mheshimiwa huyo lakini aliwapuuza kwa kuwa alikwenda kwa kazi yake ya sanaa.
“Kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu ambaye ndiye muhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?
“Ukweli mimba yangu siyo ya waziri, ifahamike kuwa namheshimu sana mheshimiwa, najisikia vibaya mtu anapoeneza kitu cha namna hiyo,” alisema Aunt kwa uchungu mkubwa.
Aunt alitiririka kwamba, mbali na uvumi huo, pia alishangazwa na baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.
“Hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?
“Wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,” alisema Aunt.
Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye pia ni mbunge.
Mbali na waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimba kubwa aliyonayo si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo kama wengi wanavyodai.
Kuhusu hilo, GPL lilizungumza na Mose Iyobo ambaye alisema kuwa anachojua ujauzito ni wa kwake lakini akashangazwa na uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu.
Swali ni je , kama Aunt anamruka Mose Iyobo na amekasirishwa na tetesi za kuhusishwa na waziri huyo ambaye ni mume wa mtu huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kufungwa Dubai, je, mimba hiyo ni ya nani?

Friday, 6 February 2015

[ Zari Hassan kufunga ndoa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, "Asema hakuna umri maalumu wa Kuoa au Kuolewa

WAKATI mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ akiwa nchini India kwa matibabu ya tatizo la kiafya linalodaiwa kuwa ni kupooza, hapa Bongo dalili za Diamond na mpenzi wa