This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday 23 July 2015

TARIBO WEST AKIRI ALIKUA ANATUMIA UCHAWI KUCHEZA SOKA

Mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Supper Eagles, hivi karibuni alitoa ushuhuda wa ajabu na kuwashtua watu wengi.
Taribo West ambaye alikuwa ni kivutio sana uwanjani enzi za ujana wake akiwa na Supper Eagles sasa ameokoka na kuwa mchungaji.
Taribo alishuhudia kwamba alikuwa akipelekwa na meneja wake nchini Senegal kwa waganga wa kienyeji ili aupige mwingi uwanjani.
Taribo West anasema alikatwa baadhi ya sehemu za ulimi, vidole na kisha kupikwa jikoni pamoja na mambo mengine ili acheze vizuri akiwa uwanjani.
Beki huyo wa zamani wa kutumainiwa wa Nigeria ambaye amekuwa ‘Pastor’ hivi sasa anasema alitembelewa na mwanamke wa Mungu, ajulikanaye kama sister Ikemefunwa akiwa nchini Italia, na kisha kumuombea na kuutoa uchawi wote na kumuweka mtu safi.
Baada ya kumaliza soka, Taribo West sasa anamtumikia Mungu kwa kutangaza maneno yake.

Tuesday 14 July 2015

MZEE YUSUPH AMESEMA INABID AACHE MZIKI KABISA

Lazima niache muziki- Mzee Yusup Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amefunguka na kusema kuwa lazima aache muziki na kufanya kazi zingine nje ya muziki

Mzee Yusuph alisema hayo alipohojiwa na mtangazaji wa Tam Tam za Mwambao ya East Africa Radio, Mwanne Othman.
Mzee Yusuph alisema kuwa kwa sasa anataraji kutoa album mbili za mwisho ili aweze kuachana na muzuki kwa swababu ana mambo mengi ya kufanya hasa siasa na kazi zake na badala yake atakuwa boss tu kwa wasanii wenzake katika kundi lake hilo ila si uimbaji tena.
"Muda ikifika nitaacha, lazima niache muziki kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya nje ya muziki, na kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nicahgue moja itabidi kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja vivyo wapenzi wa muziki wangu lazima waelewe kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine ambazo ni nyingi na zinahitaji uwepo wangu hivyo lazima niache muziki ili niweze kukamilisha mambo mengine nikiwa nje ya muziki."
Lakini mzee Yusuph aliweza kuweka wazi suala la yeye kutaka kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Fuweni Zanzibar na kusema kuwa anataka kulipa fadhila kwa namna ambavyo mashabiki wake walivyoweza kumpenda na kumjali na kuweza kumfanikishia mambo mengi kupitia njia ya muziki, hivyo yeye anaamini ubunge ni wito anaona bora awe mbunge ili jamii iweze kumtuma na kuwawakilisha wananchi katika mambo yao kwa kuwa wananch9o hao wameweza kumletea mabadiliko katika maisha yake ya kawaida.
Mbali na hilo Mzee Yusuph ameeleza kuwa yeye kuingia katika siasa si lengo ya kutafuta kutoka kimaisha bali anaamini anaweza kuwafanya jambo wananchi kwa kujitolea maana lengo lake ni kuwatumikia wananchi.
"Mimi sina ndugu sina baba ambaye ni kiongozi bali nimeingia katika siasa ili wananchi waweze kunituma maana mimi naamini hii kazi ni ya wito tu hivyo wananchi wasiangalie majina ya viongozi bali waangalie mtu mwenye dhamira njema ya kutaka kufanya jambo kwa manufaa ya wananchi na kwa kujitolea. Mimi naanzia kwenye ubunge ikiwezekana huko baadaye mpaka kwenye urais nitafika tu"

DILI LA STERLING KWENDA MANCHESTER CITY LIMETICK

Sakata hili lililoteka hisia za mashabiki duniani kote ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, limefikia tamati wakati ambao timu zinajiandaa na msimu mpya. Juzi Raheem Sterling alitajwa kwenye kikosi kitakacho safiri na kikosi cha Liverpool kuelekea kwenye mechi za pre-season, jana zikatoka habari kwamba hatasafiri na kikosi hicho.
Leo hii hatimaye klabu za Liverpool na Manchester City zimefikia makubaliano katika sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling na kutua City kwa ada ya uhamisho wa pauni 49m.
Katika makubaliano baina ya vilabu hivyo vya uingereza, Manchester City watalipa pauni 45m kwanza na kisha kuongeza pauni 4m kutokana na ushiriki wa Raheem katika kikosi hicho za Manchester.
Liverpool walikataa ofa ya kumuuza mchezaji huyu kwenda City zaidi ya mara mbili huku wakikomaa kupata pauni 50m kwa kijana huyu mwingereza mwenye asili ya Jamaica.
Sterling ambae majuma kadhaa yaliyopita alitajwa kama mmoja wa wanandinga wenye thamani zaidi chipukizi, amewachukiza sana mashabiki wa Liverpool ambao wanamuona dogo huyo kuwa mkosa adabu na heshima kwa klabu.
Aidha nahodha aliyeondoka kikosini hapo dirisha hili, Steven Gerrard amekaririwa akimlaumu mchezaji huyo kwa kukosa subira ya mafanikio ndani ya Liverpool na kuhofia kwamba litakua si jambo jema kwa Raheem kukaa benchi Manchester City wakati anapata nafasi kikosi cha kwanza, akiwa na Liverpool

HAYA SASA KWA WALE WA CHELSEA , MOURINHO ANATAKA SAINI YA HUYU NYOTA WA BARCELONA

Mwanzoni kabisa wa kipindi cha usajili Jose Mourinho alisema kwamba kwenye kipindi hiki cha usajili hatafanya sana usajili kwasababu anakikosi kizuri. Lakini pia alisema atafanya usajili mdogo tu kuziba sehemu ambazo anadhani zinahitaji usajili.
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amepanga kuwania saini ya mshambuliaji Mhispania, Pedro Rodriguez anayekipiga Fc Barcelona kwa ada ya pauni milioni 22.
Pedro ambaye hafurahii maisha hivi sasa kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Ulaya. Mfumo wa sasa wa 4; 3; 3 unamnyima nafasi Pedro kutokana na uwepo wa Messi, Suarez na Neymar.
Gazeti la Sports la nchini Uhispania linaripoti kuwa kijana huyo hatakiwi katika kikosi hicho na hivyo anaweza kuondoka katika majira haya ya joto.

Inaelezwa kuwa Barcelona wako tayari kumuachia mshambuliaji huyo kwa ada ya pauni 22m.
Pedro ambaye hapati nafasi hivi sasa katika kikosi cha Barcelona anaamini anaweza kupata dakika nyingi za kucheza tofauti na ilivyo sasa Camp Nou.
Kuelewana kwa ushirikiano wa washambuliaji watatu wa kiwango cha dunia, Messi, Suarez na Neymah unamfanya kocha wa Barcelona, Luiz Enrique kutomuangalia Pedro.

wazazi wa Iker Cassilas wamchana Florentino Perez ....

Wazazi wa Iker Casillas wamesema kuwa, kuondoka kwa mtoto wao katika klabu yake pendwa ya Real Madrid ni kutokana na kampeni chafu inayoendelea kutoka kwa rais wa klabu hiyo Florentino na kusisitiza kuwa, mtoto wao alipaswa kumalizia maisha yake ya soka katika klabu yenye hadhi ya juu na si kama klabu aina na Porto.
“Mbona wakati wa marais Lorenzo Sanz na Ramon Calderon, alikuwa akilelewa vema,” waliiambia El Mundo.
“Lakini Florentino Perez kamwe hakumpenda. Rais huyu kamwe hajawahi kumpenda, sababu kubwa ni kutokana na ufupi wake”.
“Iker amekumbana na mambo mengi ambayo hayajawahi kuandikwa. amepata matatizo makubwa ya kisaikolojia na amekuwa akichukuliwa tofauti na wachezaji wengine. Amekuwa ni kiungo muhimu sana ndani ya miaka mitano iliyopita lakini imekuwa ni suala tofauti kabisa na wanavyomfanyia hapa.”
Mama yake, Maria del Carmen Fernandez, aliongeza: “Florentino Perez ndio chanzo kikubwa sana kwa Iker kuondoka hapa Madrid. Ndio, ni kweli mwanangu amekuwa akipata ofa nyingi sana, lakini Florentino hakutaka yeye aende kwenye vilabu vikubwa. Hataki mwanangu afanikiwe.
“Porto ni timu ambayo iko katika levo sawa na timu ya daraja la pili ya Segunda B, mwanangu anahitaji timu iliyo juu zaidi ya hapo kama Barcelona.
“Kipa bora wa dunia hawezi kumalizia maisha yake ya soka katika klabu  kama ya Porto! Nisingekasirika kama mwanagu angeenda Barcelona kwa sababu ni timu bora.”
Jose Luis Casillas anahisi kuwa sehemu kubwa ya vyombo vya habari vilikuwa vikimsapoti Perez kumuandama mlinda mlango huyo mkongwe.
“Kampeni hii chafu ilinza kuundwa na Florentino huku akipewa sapoti na na baadhi ya waandishi na vyombo vya habari tangu mwaka 2010.”

50 cent hatarini kufilisika

Moja ya wasani maarufu duniani na nyota wa miondoko ya hiphop, rapa 50 Cent , aomba sheria ya kufilisika yenye kifungu cha 11 imlinde na mali zake huko marekani.
Hoja hiyo ilikuja siku chache baada ya mahakama kuamuru rapa huyo alipe dola za kimarekani milioni tano kwa mwanamke aliemshitaki kwakile alichokisema kuwa aliweka video chafu mitandanoni bila ya ridha yake.
Mwanamziki huyo mwenye jina halisi la Curtis James Jackson wa tatu ameuza zaidi ya albamu milioni thelathini duniani kote

Team ya manchester united ikiwa taari kwa safari kuelekea marekani kwa maandalizi ya msimu ujao......