Tuesday 14 July 2015

wazazi wa Iker Cassilas wamchana Florentino Perez ....

Wazazi wa Iker Casillas wamesema kuwa, kuondoka kwa mtoto wao katika klabu yake pendwa ya Real Madrid ni kutokana na kampeni chafu inayoendelea kutoka kwa rais wa klabu hiyo Florentino na kusisitiza kuwa, mtoto wao alipaswa kumalizia maisha yake ya soka katika klabu yenye hadhi ya juu na si kama klabu aina na Porto.

“Mbona wakati wa marais Lorenzo Sanz na Ramon Calderon, alikuwa akilelewa vema,” waliiambia El Mundo.
“Lakini Florentino Perez kamwe hakumpenda. Rais huyu kamwe hajawahi kumpenda, sababu kubwa ni kutokana na ufupi wake”.
“Iker amekumbana na mambo mengi ambayo hayajawahi kuandikwa. amepata matatizo makubwa ya kisaikolojia na amekuwa akichukuliwa tofauti na wachezaji wengine. Amekuwa ni kiungo muhimu sana ndani ya miaka mitano iliyopita lakini imekuwa ni suala tofauti kabisa na wanavyomfanyia hapa.”
Mama yake, Maria del Carmen Fernandez, aliongeza: “Florentino Perez ndio chanzo kikubwa sana kwa Iker kuondoka hapa Madrid. Ndio, ni kweli mwanangu amekuwa akipata ofa nyingi sana, lakini Florentino hakutaka yeye aende kwenye vilabu vikubwa. Hataki mwanangu afanikiwe.
“Porto ni timu ambayo iko katika levo sawa na timu ya daraja la pili ya Segunda B, mwanangu anahitaji timu iliyo juu zaidi ya hapo kama Barcelona.
“Kipa bora wa dunia hawezi kumalizia maisha yake ya soka katika klabu  kama ya Porto! Nisingekasirika kama mwanagu angeenda Barcelona kwa sababu ni timu bora.”
Jose Luis Casillas anahisi kuwa sehemu kubwa ya vyombo vya habari vilikuwa vikimsapoti Perez kumuandama mlinda mlango huyo mkongwe.
“Kampeni hii chafu ilinza kuundwa na Florentino huku akipewa sapoti na na baadhi ya waandishi na vyombo vya habari tangu mwaka 2010.”

0 comments:

Post a Comment