Sakata hili lililoteka hisia za
mashabiki duniani kote ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, limefikia
tamati wakati ambao timu zinajiandaa na msimu mpya. Juzi Raheem Sterling
alitajwa kwenye kikosi kitakacho safiri na kikosi cha Liverpool
kuelekea kwenye mechi za pre-season, jana zikatoka habari kwamba
hatasafiri na kikosi hicho.
Leo hii hatimaye klabu za
Liverpool na Manchester City zimefikia makubaliano katika sakata la
usajili wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling na kutua
City kwa ada ya uhamisho wa pauni 49m.
Katika makubaliano baina ya
vilabu hivyo vya uingereza, Manchester City watalipa pauni 45m kwanza na
kisha kuongeza pauni 4m kutokana na ushiriki wa Raheem katika kikosi
hicho za Manchester.
Liverpool walikataa ofa ya
kumuuza mchezaji huyu kwenda City zaidi ya mara mbili huku wakikomaa
kupata pauni 50m kwa kijana huyu mwingereza mwenye asili ya Jamaica.
Sterling ambae majuma kadhaa
yaliyopita alitajwa kama mmoja wa wanandinga wenye thamani zaidi
chipukizi, amewachukiza sana mashabiki wa Liverpool ambao wanamuona dogo
huyo kuwa mkosa adabu na heshima kwa klabu.
Aidha nahodha aliyeondoka
kikosini hapo dirisha hili, Steven Gerrard amekaririwa akimlaumu
mchezaji huyo kwa kukosa subira ya mafanikio ndani ya Liverpool na
kuhofia kwamba litakua si jambo jema kwa Raheem kukaa benchi Manchester
City wakati anapata nafasi kikosi cha kwanza, akiwa na Liverpool
0 comments:
Post a Comment