Saturday 24 January 2015

Majambazi Yaitikisa Zanzibar


Saturday, January 24, 2015

Majambazi Yaitikisa Zanzibar


Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa machinga walioko darajani Zanzibar  wamefankiwa kuwakamata majambazi wawili  huku kukiwa na taarifa kuwa mmoja amefariki baada ya kutupiana risasi  na kusababisha kizaazaa cha aina yake mjini Zanzibar.

 

Hali hiyo imetokea baada ya  polisi  kuanza  kuwasaka na kuyafuata majambazi hayo ambayo baada ya kuona wamenaswa  wakaamua kukimbia na kuingia maeneo ambayo yanatumiwa na wafanyabishara  wadogo wadogo maarufu kwa jina la  'dada njoo'.

  

Baada ya kuingia katika maeneo hayo, ndipo wafanyabishara hao wakaanza kuwanasa nakuwabana majambazi hao yaliokuwa katika gari aina ya Noah yenye namba  za usajili ambazo inasemekana ni za bandia.

 

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Muccadam Khamis amesema polisi bado inawasaka wengine ingawa amesema uchunguzi unaendelea  na kuthibitisha kuwepo kwa wananchi wanane ambao walipatwa mshtuko na wako hopitali ya Mnazi Mmoja  wakipata  huduma za matibabu.

  

Hata hivyo taarifa zilizopatikana mjini Zanzibar zinadai kuwa jambazi moja ambaye anajulikana kwa jina la Khmais Mabunduki na ambaye alikuwa anasakwa na polisi kwa muda mrefu ndiye aliyefariki kutokana na mapigano hayo, huku bado polisi wakiendelea kuwasaka wengine ambao wako katika mtandao mmoja.

0 comments:

Post a Comment