Kumekuwa na vitendo kadhaa vya kuwatilia mashaka wanamichezo wa kike
hasa pale wanapokuwa na uwezo mkubwa kuliko kawaida na mashaka zaidi
hutiliwa kwenye uhalisia wa jinsi zao ambapo wengi huhofiwa kuwa si
wanawake halisi bali ni wanaume .
Hii iliwahi kumkuta mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya na
safari hii imemkuta mwanasoka toka Nigeria Genoveva Anonma ambaye katika
hali ya kuhuzunisha alidhaniwa kuwa mwanaume .
Mbaya zaidi ni kwamba Genoveva alikutana na kadhia hii toka kwa Waafrika
wenzie ambao ni viongozi wa mamlaka kuu za soka Afrika ambao walidhani
binti huyu anadanganya kuhusu jinsia yake ya kike .
Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea alilazimishwa
kuvua nguo na kukaguliwa ili kuthibitisha kuwa ni msichana na si mvulana
kama ilivyokuwa inahofiwa nah ii ni kutokana na nguvu ambazo anazo
akiwa uwanjani na ubora alioonyesha .
Genoveva akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa alidhani kuwa
uthibitisho wa insi hufanywa hospitalini na alidhani angeitwa
hospitalini lakini cha kushangaza ni kwamba alilazimishwa kuvua nguo na
kukaguliwa jambo ambalo anakiri kuwa lilimsababishia fedheha na hasira.
Kashfa hii ilianzishw akwenye muichuano ya kombe la mataifa ya Afrika
kwa kina mama ambapo viongozi wa Ghana , Nigeria na Afrika Kusini
walizusha hoja kuwa wachezjai watatu wa Equatorial Guinea ni wanaume na
si wanawake .
Hofu hii iliondolewa baada ya wachezaji hawa kiukaguliwa na kugundulika kuwa wanawake halisi .
0 comments:
Post a Comment