This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday, 24 January 2015

MATOKEO KOMBE LA FA MPAKA SASA......

Matokeo ya michuano ya FA jumamosi kufiki sasa
Blackburn 3 - 1 Swansea FT
Birmingham 0 - 2 West Brom L
Cardiff 1 - 0 Reading L
Chelsea 2 - 1 Bradford L
Derby 1 - 0 Chesterfield L
Man City 0 - 0 Middlesbrough L
Preston 1 - 0 Sheff Utd L
Southampton 2 - 3 Crystal Palace L
Sunderland 0 - 0 Fulham L
Tottenham 1 - 0 Leicester L

Rais Kikwete awateua mawaziri 8 Tanzania

Rais Jakaya kikwetu wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.
Rais Kikwete anatarajiwa kuwaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo litakalorushwa hewani na runinga ya taifa

MAMBO YA KUZINGATIA UKIWA NA UJAUZITO

Ujauzito ni safari ndefu inayomchukua mwanamke miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua. Ni safari yenye mikikimikiki na hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito kama jambo la kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke.

Ujauzito siyo hali ya hatari au kutisha endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi cha ujauzito hadi baada kujifungua. Katika kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.
Katika makala haya tutazungumzia mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kubeba mimba, siyo kila mwanamke anaweza kubeba mimba kwa sababu wengine huwa na matatizo katika mfumo wao wa uzazi, aidha homoni zao hazifanyi kazi vizuri na mayai hayazalishwi au hayapevuki.
Huenda pia mirija ya uzazi imeziba au ana matatizo ndani ya kizazi.

NINI CHA KUFANYA?
Ni vyema upange sasa unataka kuwa mjamzito au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo, hakikisha umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako.
Mshirikishe mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri kushtukiza kwani inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja wenu hajajiandaa kisaikolojia.

CHEKI AFYA YAKO
Hakikisha una afya njema, huna magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo, kansa, HIV, kifafa, pumu, siko seli au grupu lako la damu ni RH negative.Endapo una matatizo haya hapo juu, basi haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe yatamwathiri mtoto.

Hakikisha huna magonjwa au matatizo katika viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu mbaya, vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri, matatizo katika mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
VILEVI ACHA
Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto.
Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya Folic Acid, ni vema ule sana mboga za majani au upate virutubisho vya Folic Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic Acid, kuna hatari ya kuzaa watoto wenye matatizo.

MAZOEZI
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.

YANAYOKWAMISHA UJAUZITO
Matatizo yanayoweza kukusababishia usipate mimba ni kutofahamu siku za kupata mimba, kuziba mirija ya uzazi.Pia uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi na kwenye vifuko vya mayai. Uvimbe wa aina hii unaweza kutibika kwa dawa na ukaisha au kwa njia ya upasuaji, inategemea na daktari wako atakavyoona na kuamua.

Kwa upande wa wanaume wanaojiandaa kuwa wazazi, ni vema umjulishe mpenzi wako sasa unataka mtoto au lini unataka mtoto. Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa uzazi, mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa manii zote zinatoka ukeni.
Ni vema ukapime mbegu zako za kiume kuona kama zina ubora wa kutosha, usiwe na maumivu yoyote ya mwili kwani yataweza kukusababishia kupunguza nguvu za kiume na kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Nigeria (nollywood) nao wafanya madudu kama bongo movies.......

            whats Wrong With This Photo from Nigerian Movies?! wavaa nguo za ajabu ambazo ziko nje ya maadili..... af zaidi ukiangalia kwa nyuma kuna kioo ambacho kinaonesha wapiga picha na watu wengine ambao sio sehemu ya kipande hichi cha movie

TIKO AWAVAA WANAUME!!!


Saturday, January 24, 2015

Tiko Awavaa Wanaume Wanaodai yeye ni GOGO Kitandani


Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Tiko Hassan amesema hakuna kauli ambayo haipendi kama kuambiwa si hodari wa mapenzi (gogo) wakati anajiamini yupo vizuri katika sekta hiyo.

Tiko alifunguka kauli hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wetu na lilipofika suala la malovee, Tiko aling’aka vibaya mara baada ya kuambiwa kuwa kuna marafiki zake wanamuita gogo.

 

“Wee nani kasema? Sipendi kuitwa hivyo wakati mwenyewe najijua kabisa ninakuwaje pindi ninapokuwa na mpenzi wangu, najiamini kweli,” alisema Tiko

Majambazi Yaitikisa Zanzibar


Saturday, January 24, 2015

Majambazi Yaitikisa Zanzibar


Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa machinga walioko darajani Zanzibar  wamefankiwa kuwakamata majambazi wawili  huku kukiwa na taarifa kuwa mmoja amefariki baada ya kutupiana risasi  na kusababisha kizaazaa cha aina yake mjini Zanzibar.

 

Hali hiyo imetokea baada ya  polisi  kuanza  kuwasaka na kuyafuata majambazi hayo ambayo baada ya kuona wamenaswa  wakaamua kukimbia na kuingia maeneo ambayo yanatumiwa na wafanyabishara  wadogo wadogo maarufu kwa jina la  'dada njoo'.

  

Baada ya kuingia katika maeneo hayo, ndipo wafanyabishara hao wakaanza kuwanasa nakuwabana majambazi hao yaliokuwa katika gari aina ya Noah yenye namba  za usajili ambazo inasemekana ni za bandia.

 

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Muccadam Khamis amesema polisi bado inawasaka wengine ingawa amesema uchunguzi unaendelea  na kuthibitisha kuwepo kwa wananchi wanane ambao walipatwa mshtuko na wako hopitali ya Mnazi Mmoja  wakipata  huduma za matibabu.

  

Hata hivyo taarifa zilizopatikana mjini Zanzibar zinadai kuwa jambazi moja ambaye anajulikana kwa jina la Khmais Mabunduki na ambaye alikuwa anasakwa na polisi kwa muda mrefu ndiye aliyefariki kutokana na mapigano hayo, huku bado polisi wakiendelea kuwasaka wengine ambao wako katika mtandao mmoja.