Saturday 24 January 2015

Rais Kikwete awateua mawaziri 8 Tanzania

Rais Jakaya kikwetu wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.
Rais Kikwete anatarajiwa kuwaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo litakalorushwa hewani na runinga ya taifa

0 comments:

Post a Comment