This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Thursday, 23 July 2015
TARIBO WEST AKIRI ALIKUA ANATUMIA UCHAWI KUCHEZA SOKA
Tuesday, 14 July 2015
MZEE YUSUPH AMESEMA INABID AACHE MZIKI KABISA
Lazima niache muziki- Mzee Yusup Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amefunguka na kusema kuwa lazima aache muziki na kufanya kazi zingine nje ya muziki
Mzee Yusuph alisema hayo alipohojiwa na mtangazaji wa Tam Tam za Mwambao ya East Africa Radio, Mwanne Othman.Mzee Yusuph alisema kuwa kwa sasa anataraji kutoa album mbili za mwisho ili aweze kuachana na muzuki kwa swababu ana mambo mengi ya kufanya hasa siasa na kazi zake na badala yake atakuwa boss tu kwa wasanii wenzake katika kundi lake hilo ila si uimbaji tena.
"Muda ikifika nitaacha, lazima niache muziki kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya nje ya muziki, na kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nicahgue moja itabidi kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja vivyo wapenzi wa muziki wangu lazima waelewe kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine ambazo ni nyingi na zinahitaji uwepo wangu hivyo lazima niache muziki ili niweze kukamilisha mambo mengine nikiwa nje ya muziki."
Lakini mzee Yusuph aliweza kuweka wazi suala la yeye kutaka kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Fuweni Zanzibar na kusema kuwa anataka kulipa fadhila kwa namna ambavyo mashabiki wake walivyoweza kumpenda na kumjali na kuweza kumfanikishia mambo mengi kupitia njia ya muziki, hivyo yeye anaamini ubunge ni wito anaona bora awe mbunge ili jamii iweze kumtuma na kuwawakilisha wananchi katika mambo yao kwa kuwa wananch9o hao wameweza kumletea mabadiliko katika maisha yake ya kawaida.
Mbali na hilo Mzee Yusuph ameeleza kuwa yeye kuingia katika siasa si lengo ya kutafuta kutoka kimaisha bali anaamini anaweza kuwafanya jambo wananchi kwa kujitolea maana lengo lake ni kuwatumikia wananchi.
"Mimi sina ndugu sina baba ambaye ni kiongozi bali nimeingia katika siasa ili wananchi waweze kunituma maana mimi naamini hii kazi ni ya wito tu hivyo wananchi wasiangalie majina ya viongozi bali waangalie mtu mwenye dhamira njema ya kutaka kufanya jambo kwa manufaa ya wananchi na kwa kujitolea. Mimi naanzia kwenye ubunge ikiwezekana huko baadaye mpaka kwenye urais nitafika tu"
DILI LA STERLING KWENDA MANCHESTER CITY LIMETICK
HAYA SASA KWA WALE WA CHELSEA , MOURINHO ANATAKA SAINI YA HUYU NYOTA WA BARCELONA
wazazi wa Iker Cassilas wamchana Florentino Perez ....
50 cent hatarini kufilisika
Mwanamziki huyo mwenye jina halisi la Curtis James Jackson wa tatu ameuza zaidi ya albamu milioni thelathini duniani kote
Friday, 27 March 2015
Rooney : sitashangilia tena kwa mtindo wa boxing
HUYU NDIO MBUNGE MZURI ZAIDI TANZANIA...... BONGO MOVIES WOTE WANAKAA CHINI ANIII...... jina lake Catherine Magige
Catherine Magige Mbuge wa Arusha atajwa kua mbunge mzuri zaidi,, ana mvuto wa sura,, shape analo yuko vizuri aseeeeee!!!!! Ukimuangalia fasta fasta bila kuambiwa anafanya kazi gani,, utasema anacheza sinema za Bongo movies lakini lahashaa. Yeye ni mbunge mwenye mvuto wa aina yake... yuko smart, photogenic, na sifa nyingine nzuri ni nouma sanaaaaaa
Agness Masogange atwajwa kua mwanamke mzuri zaidi TANZANIA
Friday, 20 February 2015
Huyu ndiye mkuu mpya wa wilaya ya Iramba mh. LUCY MAYEMBA aliyeteuliwa na J.K. Sema neno lolote kwa uteuzi huu
Huyu ndiye mkuu mpya wa wilaya ya Iramba mh. LUCY MAYEMBA aliyeteuliwa na J.K.
Sema neno lolote kwa uteuzi huu
Wanasayansi wamegundua kwamba wanaume walio wakarimu na wanaowasikiza wake zao kidole chao cha nne ni kirefu ikilinganishwa na kidole chao cha pili
Wanasayansi wamegundua kwamba wanaume walio wakarimu na wanaowasikiza wake zao kidole chao cha nne ni kirefu ikilinganishwa na kidole chao cha pili.
Je, unakubaliana na utafiti huu uliofanywa na wanasayansi katika chuo kikuu cha McGill University nchini Canada.
Thursday, 19 February 2015
FUNDI SAA APOKEA KICHAPO BAADA YA KUDAIWA KUMLAWITI MTOTO HUKO ARUSHA
Mapigano ya Magaidi na Polisi Mapango ya Amboni Tanga Hii ndio..........
Mapigano ya Magaidi na Polisi Mapango ya Amboni Tanga Hii ndio Full Story
NI kama kumekucha! Siku chache tu baada ya Gazeti la Ijumaa (ndugu na hili) kuandika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; Kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini...NI HUYU, kundi jingine limeibuka na kuandika mkanda wa video wakizungumzia uhalifu....Cha ajabu, sanjari na kundi hilo linalodai liko Tanga, Tanga hukohuko kwenye Kitongoji cha Amboni, Ijumaa iliyopita kulizuka mapigano kati ya polisi, askari wa JWTZ wakipambana na kundi lililodhaniwa ni la kigaidi likiwa limepiga makazi ndani ya mapango ya kihistoria ya Amboni, Uwazi lina full story.
Katika mapigano hayo hadi juzi Jumapili, askari mmoja wa JWTZ aliuawa huku wanajeshi watatu na askari polisi wawili wakijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.
MASHUHUDA WA MAPIGANO
Kabla Uwazi halijatiririka na video hiyo, lilizungumza na wananchi wenye makazi yao kwenye Kitongoji cha Amboni ambako mapigano ya askari na wahalifu yalitokea.
Mzee Ibrahimu Ally, yeye anasema: “Siku ya tukio (Ijumaa asubuhi) mimi nilikuwa nimepumzika ndani kwangu lakini ghafla nikasikia mlio wa risasi kama mara mbili hivi.
“Mke wangu alikuwa anafua, akaja mbio ndani akisema ni majambazi. Nilimwambia funga mlango haraka sana, akaufunga. Lakini cha ajabu milio ya risasi ikawa inaongezeka kadiri muda ulivyokwenda.
“Ilifika mahali nikajua si majambazi bali tumevamiwa na majeshi ya nje ya nchi. Kwani sasa risasi zilikuwa zikirindima kila muda. Hali ikawa tete kwa kweli. Hata hapa ninapoongea na wewe siamini kama ile milio ya risasi haitajirudia tena.”
WAZIKIMBIA NYUMBA
Mwanahawa Mudale yeye alisema: “Ilibidi tuhame majumba kwenda kujificha, tatizo ni ile milio ya mabomu na risasi na baadaye tukaona chopa (helikopta) ikitembea angani. Awali tulijua ni vita ya nchi na nchi, kumbe walikuwa askari wetu.”
SIKU MBILI HAKUNA KULALA
Baadhi ya mashuhuda wanasema kutokana na milio ya risasi kwa siku ya Ijumaa hadi Jumamosi asubuhi, hakuna mwananchi aliyepata usingizi.
“Mimi na familia yangu hatujalala jamani. Risasi na mabomu yasikieni hivihivi tu. Kuna wakati tulikuwa tukiona miale ya moto kutokea kwenye eneo la mapango. Wakati mwingine badala ya moto tuliona moshi mkubwa.
“Kumbe wanajeshi wetu nao walishafika kupambana na hao watu,” alisema Simeon Patrick, mkazi wa Kitongoji cha Karasha, Amboni.
INAVYODAIWA
Habari zilizosambaa juzi, zinadaiwa kundi hilo lililopambana na askari ni la kigaidi ambapo safari yao kubwa ilikuwa kwenda kufanya ugaidi wa kumwaga damu nchi jirani ya Kenya.
Wale jamaa nasikia walikuwa wakipeleka vifaa nchini Kenya eneo la mwambao ili waje wafanye uhalifu baadaye.
“Sasa wakiwa katika hatua za mwisho mwisho baada ya kupeleka silaha za kivita, wakashtukiwa. Ikabidi waache silala zao eneo walipozificha na wao waje Tanga kujificha kwenye mapango.
“Lengo lao, watulie mpaka hali kule Kenya itakapokuwa imepoa ndipo wajitokeze. Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati wanaishi mapangoni ilibidi waanze kutoka kutafuta chakula kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ndipo siku moja jamaa yao mmoja akakamatwa kwa uhalifu.
“Yule jamaa ndiye aliyewapeleka polisi walipo wenzake na kutokea kwa mapigano makali kama yale,” alisema mtoa habari mmoja huku akiomba jina lake lihifadhiwe.
WANACHOAMINI WANANCHI, TOFAUTI NA POLISI
Uwazi lilibahatika kuzungumza na baadhi ya wananchi wa jijini Tanga ambapo karibu wote walikuwa na mtazamo mmoja tu.
“Kutuambia wale ni majambazi si sawasawa. Majambazi wetu tunawajua, polisi wanawatosha sana, sasa hawa wametokea wapi mpaka JWTZ washirikishwe?” alihoji Paulina Mathias, mkazi wa Chumbageni, Tanga.
Kusema ukweli serikali ituambie moja. Lakini wale si majambazi. Kwanza mpaka leo hii (juzi) hawajamkamata hata mmoja zaidi ya kujeruhi askari wetu na kumuua mmoja. Wale ni magaidi, lazima tuwe makini sana,” alisema Ally, mkazi wa Duga Maforoni, Tanga.
KUHUSU VIDEO MPYA
Tukiachana na mapigano ya Amboni, sasa turudi kwenye video mpya ya watu waliojiita ni watetezi wa haki dhidi ya udhalimu.
Video hii ipo ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wanaonekana watu wawili wakiwa wamevaa mavazi ya kininja ili wasijulikane.
Watu hao wanasema wanapinga jamii yao kukamatwa na kuuawa mara kwa mara wakidai jeshi linawaonea hivyo kutangaza kupambana na askari.
Video hiyo haipishani sana na ile iliyotangulia kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Ijumaa.
KAULI YA JESHI LA POLISI
Akizungumza na Uwazi jijini Tanga muda mfupi baada ya kutulia kwa mapambano ya Amboni, Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na shughuli zao za kawaida huku akisisitiza:
“Askari walifika mapangoni, kundi lile ni la majambazi. Lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano, askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.
Thursday, 12 February 2015
UN yailaumu Tanzania kwa yanayotokea DRC
Serikali yaiagiza TANESCO kushusha bei ya umeme
Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Mh. George Simbachawene amelitaka shirika la umeme nchini (TANESCO) kupunguza bei ya umeme kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Soma Zaid hapa
nchi kavu na majini SUMATRA kuona uwezekano wa kupunguza bei za nauli ili wananchi waone faida ya kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Saturday, 7 February 2015
HARRY KANE WA SPURS AENDELEA KUWA TISHIO KWA TIMU KUBWA UINGEREZA........ Aipiga Arsenal...
HIVI NDIVYO ILIVYOKUA INDIA KWENYE SHOW YA DIAMOND
Rose Ndauka: Sitazaa Tena Nje ya Ndoa
Aunt: Mimba Yangu Siyo ya Waziri!
Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye pia ni mbunge.
Friday, 6 February 2015
[ Zari Hassan kufunga ndoa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, "Asema hakuna umri maalumu wa Kuoa au Kuolewa
Friday, 30 January 2015
NIPIGE MKE WANGU MAANA MDA MWINGINE NAKOSA ADABU!!
Friday, January 30, 2015
Shilole aomba radhi kwa kumdunda Nuh Mziwanda .......Nuh naye kasema yupo tayari kupigwa mpaka AKOME!!!
Baada ya Shilole kumchapa vibao mchumba wake Nuh Mziwanda, Shilole amelazimika kuomba radhi.
Shilole amewaomba radhi mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram kwa kupost picha akiwa na mpenzi wake huyo na kuandika:
“Huyu hapa mjanja wangu mimi, daah nimekamatika hapa, na naamini ni mwanaume sahihi kwangu maana hawezagi kurusha hata ngumi japo namchokozaga mie mjeuri tu, mnao muhandama mme wangu mmeshindwa, kugombana ni kawaida sana kwenye mapenzi na kama nliwaudhi mashabiki wangu mnisamehe mie nampenda mme wangu.”
Naye Nuh Mziwanda aliandika:
Mwanaume lijali aliekamilika ampigi mpenzi wake wala kurudishia kibao au kofi alilopigwa na mpenzi wake.naamini kwenye mapenzi ya kweli wivu lazima na kugombana kwenye mapenzi ni kama kwenda chooni ni swala la kawaida sana.aaaaaaaya mke wangu nimekup rukhsa nipige mpaka nikome.ila all i know its love dats it.Nawapenda Mashabiki wangu pamoja sana .#zimaTaa sie tayari
Tuesday, 27 January 2015
Ushuhuda Huu wa Mzungu Kuhusu Wauza Madawa ya Kulevya
Jan 26, 2015
Ushuhuda Huu wa Mzungu Kuhusu Wauza Madawa ya Kulevya 'Unga’ Ufanyiwe Kazi
Kwa zaidi ya wiki tatu sasa, Watanzania wamekuwa wenyeji wa mgeni ambaye ujio wake nchini umekuwa wa aina yake. Tunaweza kusema ugeni huo siyo wa kawaida, kwani tumezoea kuona ziara za wanasiasa, wafanyabiashara na wageni wengine wengi kutoka katika mataifa mbalimbali wanaokuja kwa ziara za kiserikali na nyinginezo, mbali na watalii wanaotembelea nchi yetu kujionea vivutio lukuki vilivyosambaa kila sehemu.
Hata hivyo, ziara ya Padri John Wootherspoon, raia wa Australia aliyekuja nchini Januari Mosi, mwaka huu ni tofauti kabisa na ziara nyingine tulizozizoea. Yeye anaishi China na amepata kibali cha Serikali ya China kutembelea magereza mbalimbali nchini humo na kuwafariji wafungwa. Katika kufanya kazi yake hiyo katika magereza nchini China na majimbo yake ya Hong Kong na Macau, amekutana na wafungwa wengi kutoka nchi mbalimbali duniani na kugundua kwamba kilichowaingiza magerezani ni biashara ya dawa za kulevya.
Kabla ya kuja hapa nchini, Padri Wootherspoon aliliambia gazeti hili, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likifuatilia huduma zake katika magereza nchini China kuwa, alikuwa na mpango wa kuitembelea Tanzania baada ya kugundua kwamba idadi ya Watanzania wanaotumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini China ni kubwa mno ikilinganishwa na wafungwa wengine kutoka nchi nyingine. Anasema wafungwa zaidi ya 130 kutoka Tanzania wako katika magereza ya Shek Pik, Stanley, Loo Woo na Macau na kwamba kila mwezi Watanzania wanne hadi sita wanafungwa magerezani kwa makosa hayo.
Kutokana na hali hiyo, Padri Wootherspoon aliamua kuja Tanzania kwa gharama zake mwenyewe ili kuwasaidia wafungwa hao kuwasiliana na familia zao hapa nchini, baada ya kupata mawasiliano ya familia hizo kutoka kwa wafungwa hao. Anasema wafungwa hao walitumiwa tu na wafanyabiashara wakubwa (ambao majina yao tunayahifadhi kwa sasa) kupeleka dawa hizo nchini China na kwamba tangu awasili nchini amewasiliana na familia nyingi za wafungwa hao, ambazo amesema zimo katika umaskini mkubwa. Padri huyo tayari amekutana na Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, ACP Godfrey Nzowa na kumtaka aende nchini China kupata taarifa za kina kutoka kwa wafungwa hao.
Sisi tunadhani ziara ya Padri huyo hapa nchini ni fursa ya pekee kwa Serikali kupata taarifa muhimu za kusaidia kutokomeza biashara hiyo. Juni, mwaka jana Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi alisema wakati wa kuadhimisha Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kwamba kazi ya kuwanasa vinara wa biashara hiyo imekuwa ngumu na akisema vijana wa Kitanzania 65 kati ya 403 waliokamatwa nchi za nje kwa kuhusika na usafirishaji wa dawa za kulevya wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Waziri Lukuvi pia alisema vitendo vya rushwa vimekwamisha jitihada na mikakati ya kuwatia mbaroni vigogo wa biashara hiyo. Bahati nzuri ni kwamba Padri Wootherspoon yuko nchini kama sehemu ya suluhisho la tatizo hilo.
Ni matarajio yetu kwamba Serikali itafanya kila linalowezekana kushirikiana naye ili kupata taarifa muhimu zitakazosaidia kuwakamata wamiliki wa biashara hiyo. Hatua hiyo pia itaondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi kwamba kikwazo kikuu katika vita ya kukomesha uhalifu huo kimo ndani ya Serikali yenyewe.
Mama wa Mapacha sita anunuliwa nyumba
Tuesday, 27 January 2015
Mama wa Mapacha sita anunuliwa nyumba
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akikata utepe, kuashilia uzinduzi Rasmi wa nyumba aliyokabidhiwa Salome Mhando ambaye alitelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo hadi kufikia sita na kukosa Mahali pa kuishi, Covenant Bank imemkabidhi nyumba hiyo ambayo ataimiliki yeye mwenyewe pamoja na thamani za ndani na Bima ya Matibabu kwa Mwaka mzima. Anaeshuhudia ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja (wa kwanza kushoto) na Salome Mhando (wa kwanza kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (kushoto), Pamoja na Mkurugenzi wa benki Hiyo, Sabetha Mwambenja, wakimkabidhi hati ya kiwanja na Umiliki wa nyumba Salome Mhando, Mama alietelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo, hadi kufikia sita, Benki hiyo imemkabidhi nyumba hiyo pamoja na Bima ya Matibabu kwa mwaka mzima
AIBU ILIOJE
Tuesday, January 27, 2015
AIBU: Shilole Amchapa Makofi Mpenzi wake Nuhu Mziwanda
Jumamosi iliyopita ndani ya Tamasha la Kiboko Yao lililofanyika Leaders Club, Gazeti la Makorokocho lilishudia live Msanii Shilole akimchezeshea kichapo mchumba wake Nuh Mziwanda kwa madai kuwa Nuh alikua hataki kuondoka nae eneo la tukio....
Mchekeshaji Steve Nyerere alijitokeza kuamulia ugomvi na kufanikiwa kumtoa Shilole eneo lile lakini baada ya muda Shilole akarudi na kumdai funguo ya gari Nuh ambaye siku hiyo alionekana kuwa mpole ikabidi mabaunsa waingilie kati na kumtoa kwa nguvu shilole....
Baadae Nuh alionekana akitoa machozi na Malkia wa Taarabu Khadija Kopa alionekana akimbembeleza na kumfuta machozi.
Monday, 26 January 2015
Mwanamke Awaua watoto wake wawili na Kuwazika ndani ya Nyumba Yake
Mwanamke Awaua watoto wake wawili na Kuwazika ndani ya Nyumba Yake
Mwanamke mmoja mkazi wa mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini kata ya Chemchem amewaua watoto wake wawili na kuwazika ndani ya nyumba yake.
Mwanamke huyo amedai kuwa kilichomfanya awalishe sumu watoto wake ni ugumu wa maisha uliokuwa ukimkabili baada ya kikimbiwa na mumewe.
Kwa mujibu wa jirani yake, siku ya tukio mwanamke huyo alisikika akichimba shimbo ndani ya nyumba yake kabla ya kutangaza kupotelewa na watoto wake siku ya pili yake.
Taarifa ya kupotea kwa watoto hao ilimpa mashaka jirani huyo na kumlazimu akatoe taarifa polisi ambapo maafande walikuja na kufanya msako ndani ya nyumba hiyo ambapo walifanikiwa kufukua maiti za watoto hao.
Saturday, 24 January 2015
TUKIO LA KINYAMA:MWENYEKITI AKATWA KICHWA NA SEHEMU ZA SIRI KISHA KUWEKWA KWENYE SUFURIA
KATI YA ZARI 41, NA WEMA 26.... YUPI BORA..................................... DIAMOND NDO MWENYE MAJIB
What is it about older women? I have heard it said that the key weapon in an older woman’s arsenal is that she knows how to treat a man but my response is always that a man is not a cat! A man is not feline to be kept. Men are hunters.
Then there is the usual almost cliche rebuttal that a young girl while sweet is usually a bucketload of drama. What do you think? If you were to ask Diamond, he would probably say that older ladies are sweeter. Something to do with fine wine and time but what do I know? Personally, I am one of those who believe that raw mangoes taste infinitely better because you can add pilipili and salt to them. Perhaps you like my friend Chege Miati prefer old squishy mangoes. I do not know.
But you see, Diamond dated Wema Sepetu, a young -er lass for quite some time. Sadly, that union ended when he decided to dump her the same way we through day old cold porridge outside the window the very moment he saw Zari, the 41 year old MILF.
Compare the two if you would
MATOKEO KOMBE LA FA MPAKA SASA......
Rais Kikwete awateua mawaziri 8 Tanzania
MAMBO YA KUZINGATIA UKIWA NA UJAUZITO
Nigeria (nollywood) nao wafanya madudu kama bongo movies.......
TIKO AWAVAA WANAUME!!!
Saturday, January 24, 2015
Tiko Awavaa Wanaume Wanaodai yeye ni GOGO Kitandani
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Tiko Hassan amesema hakuna kauli ambayo haipendi kama kuambiwa si hodari wa mapenzi (gogo) wakati anajiamini yupo vizuri katika sekta hiyo.
Tiko alifunguka kauli hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wetu na lilipofika suala la malovee, Tiko aling’aka vibaya mara baada ya kuambiwa kuwa kuna marafiki zake wanamuita gogo.
“Wee nani kasema? Sipendi kuitwa hivyo wakati mwenyewe najijua kabisa ninakuwaje pindi ninapokuwa na mpenzi wangu, najiamini kweli,” alisema Tiko
Majambazi Yaitikisa Zanzibar
Saturday, January 24, 2015
Majambazi Yaitikisa Zanzibar
Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa machinga walioko darajani Zanzibar wamefankiwa kuwakamata majambazi wawili huku kukiwa na taarifa kuwa mmoja amefariki baada ya kutupiana risasi na kusababisha kizaazaa cha aina yake mjini Zanzibar.
Hali hiyo imetokea baada ya polisi kuanza kuwasaka na kuyafuata majambazi hayo ambayo baada ya kuona wamenaswa wakaamua kukimbia na kuingia maeneo ambayo yanatumiwa na wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kwa jina la 'dada njoo'.
Baada ya kuingia katika maeneo hayo, ndipo wafanyabishara hao wakaanza kuwanasa nakuwabana majambazi hao yaliokuwa katika gari aina ya Noah yenye namba za usajili ambazo inasemekana ni za bandia.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Muccadam Khamis amesema polisi bado inawasaka wengine ingawa amesema uchunguzi unaendelea na kuthibitisha kuwepo kwa wananchi wanane ambao walipatwa mshtuko na wako hopitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma za matibabu.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana mjini Zanzibar zinadai kuwa jambazi moja ambaye anajulikana kwa jina la Khmais Mabunduki na ambaye alikuwa anasakwa na polisi kwa muda mrefu ndiye aliyefariki kutokana na mapigano hayo, huku bado polisi wakiendelea kuwasaka wengine ambao wako katika mtandao mmoja.