Saturday 17 January 2015

AMANDA"Staki kumtambulisha bwana wangu"!

Jan 17, 2015

Hapa na Pale:Sitaki Kumtambulisha Bwana Wangu wa Sasa, Wataniibia!-Amanda

Mwigizaji wa filamu mwenye umbo la lenye mvuto wa aina yake, Tamrina Posh ‘Amanda’ amefunguka kuwa anaogopa kumtambulisha bwana wake wa sasa kwa kile alichodai kuwa anaogopa kuibiwa.

Akizu ngumza na paparazi wa GPL juzikati, Amanda alisema ameishi kwa muda mrefu na mpenzi wake bila kuhitilafiana kwa sababu wengi hawamjui, lakini anahofia akimuanika wasichana wataanza kumfuatafuata na kumwiba.

“Kumtambulisha bwana wangu wa sasa sitaki, naogopa wadada wa mjini hawakawii kumzengea zengea na kuniibia hivihivi naona. Kwa mfano sasa hivi watu hawamjui basi wametuliaaa! Lakini ukimweka hadharani tu, hao,” alisema Amanda.

0 comments:

Post a Comment