Monday, 19 January 2015

UONGOZI WA ARSENAL WAZURU KWA KUENDELEZA SOKA NCHINI

Monday, 19 January 2015

UONGOZI WA ARSENAL WAZURU KWA KUENDELEZA SOKA NCHINI

 Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

Uongozi  wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza umezuru Tanzania kwa ajili kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Uhusiano na Maendeleo wa timu  hiyo ,Sam Stone amesema kuwa Tanzania ni  nchi ya sita kwa ukubwa katika bara la Afrika hivyo watasaidia katika kukuza soka nchini.

Amesema kesho watakuwa na mazungumzo na Rais wa Shirikisho la  Mpira wa Miguu nchini (TFF),Jamal Malizi juu ya uendeleza soka nchini.

Amesema katika ziara hiyo wanatarajia kukutana na makampuni 20 kwa ajili ya masuala ya biashara katika kuongeza uwigo zaidi kati timu na wadau wengine katika nchi ya Tanzania .

Kwa upande wa Meneja wa Uhusiano na Maendeleo wa timu ya Arsenal Daniel Willey amesema wataendelea kutafuta wadau zaidi na kuendeleza soka nchini kwani Tanzania ni nchi ambayo ni kubwa inaweza kwenda mbele katika mafanikio ya soka.

Afisa Mtendani Mkuu wa Kampuni ya EAG Group,Iman Kajura (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akiutambulisha Uongozi  wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza,ulikuja Tanzania kwa ajili kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini.Mkutnao huo umefanyika kwenye hoteli ya Southansun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Maendeleo wa Timu ya Soka ya Arsenal,Sam Stone na katikati ni Meneja Mahusiano na Maendeleo wa timu hiyo,Daniel Willey.

0 comments:

Post a Comment