Saturday 17 January 2015

Ushindi wa UNITED vs QPR



EPL: Hiki ndicho kilichojiri kwenye mechi ya Man United vs QPR

Posted by: Sports TZAJanuary 17, 2015Michezo

Baada ya kutoshinda kwenye ligi kuu ya England kwa mechi 3 mfululizo- wakitoka sare mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Saints, leo hii vijana wa Louis van Gaal walisafiri hadi London kwenda kukipiga na Queens Park Rangers.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Loftus Road umemalizika hivi punde na matokeo ya mchezo ni ushindi wa taabu kwa mashetani wekundu.

Magoli ya wachezaji waliotokea benchi Maroune Fellaini na James Wilson yaliokoa jahazi la United ambalo lilibebwa tena na uwezo mkubwa wa kuzuia michomo wa David De Gea.

Kwa ushindi wa leo United wamepanda hadi nafasi ya 3 mbele ya Southampton ambao muda huu wapo uwanjani wakipambana na Newcastle

0 comments:

Post a Comment