Sunday 18 January 2015

BOLT KUTUA TZ

USAIN BOLT KUTUA TZ

KWA UFUPI

“Kuanzishwa kwa mbio za FBI lilikuwa ni wazo langu na Franken, japo awali sikutaka kulifanya kutokana na tofauti niliyokuwa nayo na Bayi na Nyambui japo mwandaaji hakuwahi kujua tofauti hiyo.

SHARE THIS STORY

 Tweet 

 0
inShare

Dar es Salaam. Mwanariadha nyota na bingwa wa dunia wa mita 100, Usain Bolt  kutoka Jamaica amealikwa kushiriki mbio za kimataifa za FBI zitakazofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

Mbio hizo zimeandaliwa na mwandaaji wa kimataifa, Al Franken na mwanae Don zikilenga kumuenzi mwanariadha wa zamani, Filbert Bayi ambaye aliweka rekodi kwenye mbio za maili moja ambazo zimeitwa Miracle Mile.

Tayari, maandalizi ya mbio hizo yameanza na zitafanyika kwa usimamizi wa Shirikisho la Riadha la Dunia (IAAF), Riadha Tanzania (RT), klabu ya michezo ya Hanang na Taasisi ya Filbert Bayi (FBF).

Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa klabu ya Hanang Wilhelm Gidabuday alisema lengo la mbio hizo ni kuwaenzi wanariadha waliowahi kuiletea sifa nchi na kusisitiza kuwa tayari amemaliza tofauti yake na Bayi na Suleiman Nyambui kwa manufaa ya Taifa.

“Kuanzishwa kwa mbio za FBI lilikuwa ni wazo langu na Franken, japo awali sikutaka kulifanya kutokana na tofauti niliyokuwa nayo na Bayi na Nyambui japo mwandaaji hakuwahi kujua tofauti hiyo.

“Hata hivyo, sikuona sababu ya kuendelea na mgogoro huo na kulazimika kuweka tofauti zetu pembeni na tayari nimezungumza na Bayi na Nyambui nao wameridhia mbio hizi zifanyike,” alisema Gidabuday.

Alisema kuwa tayari Franken ameridhia mbio hizo zifanyike Tanzania na ameeleza kuwaleta nyota wa riadha wa dunia akiwamo Bolt, raia wa Jamaica anayetamba kwenye mbio fupi za mita 100, 200 na 400.

“Mbio za FBI zitakuwa za viwanjani kuanzia mbio za mita 100 hadi 10,000, kinachofanyika ni kuziombea IAAF ili ziwe katika orodha ya mbio kubwa za kimataifa,” alisema.

0 comments:

Post a Comment