Sunday 18 January 2015

Usafishaji wa dawa za kulevya

Jan 18, 2015

Usidanganywe Kupeleka Madawa ya Kulevya Miji Hii, Ukikamatwa Unapigwa Risasi

Nimesikitishwa sana na orodha ndefu ya vijana wanaoshikiliwa na wengine wameshatolewa hukumu ya kunyogwa wengi wao ni kutoka Tanzania, lakini hii inatokana na vijana wengi wa kitanzania kudanganywa kwa kutaka utajiri wa haraka haraka.

Usijaribu wala usidanganywe kupeleka madawa ya kulevya hasa katika miji ya Macao, Hongkong,Indonesia, maana ni hatari sana kwani kifungo cha chini kabisa kwa gram moja ni 7 years,ila wengi uhukumiwa kwa kunyogwa na kifungo cha maisha na kazi ngumu.

Matajiri wengi uwadanganya vijana matokeo yake uishia magerezani na kunyongwa.

Jana Indonesia imewapiga risasi raia wa nchi tano zikiwemo zenye nguvu kiuchumi kwa raia wake kuingiza madawa ya kulevya nchini humo,licha ya nchi hizo kuwaita nyumbani mabalozi wake.

Jamani usidanganywe heti utafungwa miaka 2 utatoka, matajiri waelezeni ukweli kabla ya kuwatuma huko, mimi nilikuwa mji wa Macau ukweli hali inasikitisha kwa watanzania wanateseka sana.

0 comments:

Post a Comment